Kukabiliana na njia panda
Facing A Crossroads – SWA
“Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA,chagueni hivi leo mtakayemtumikia;kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngámbo ya Mto au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao;lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.” (Yoshua 24:15)
Katika kitabu cha 1 Wafalme 18 tunaona jinsi taifa la Israeli lilipokuwa limefikia njia panda.Halikumheshimu tena Mungu.Kwao,huyo Mungu alikuwa umbali wa maili mamilioni kadhaa.Japo waliendelea kusema ni wafwasi wa Yehova,lakini ukweli ni kwamba hakuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.Hata hivyo Mungu alijua kwamba alihitaji kuwakumbusha tu kuhusu uweza wake,ambao ungeliwaamsha kutoka kwenye usingizi wao wa kiroho.Kwa hivyo Mungu alimtumia Eliya kuleta mabadiliko katika maisha yao.Huku akikabiliwa na vipingamizi-mtu mmoja dhidi ya mamia ya viongozi wapagani-Eliya alidhihirisha bayana nguvu za Mungu.
Katika kitabu chicho hicho wa 1 Wafalme 18:22-39,watu walishuhudia ushindani wa ajabu.Kuliandaliwa mioto mara mbili tofauti ya kuni ,ambapo mafahali wawili waliokatakatwa waliwekwa juu yake kama sadaka ya kuteketezwa.Ni Mungu yupi aliyekuwa na uwezo wa kuasha moto kwenye mojawapo wa madhabahu hayo-Baali au Mungu wa Eliya?
Eliya kwa ujasiri mkuu uliotokana na imani katika Mungu mkuu,aliwatazama manabii 850 wapagani wakiomba miungu yao iwashe moto kwenye rundo lao kwenye madhabahu,lakini hapakuwaka moto.Eliya aliwakebehi na kuwaambia wawaite miungu wao kwa sauti ya juu labda wamelala!Kwa saa kadhaa manabii hao walipaaza sauti na hata kujikatakata kwa visu na vyembe na damu kuwachuruzika,lakini hapakutokea ishara ya moto.
Basi Eliya akatokea na kusogelea madhabahu yake ambako kulikuwa na dhabihu ya ng’ombe waliokatakatwa.Aliyafanyia matengenezo madhabahu hayo yaliokuwa yametelekezwa na wana wa Israeli.Aliyatwaa mawe kumi na mawili yalioakilisha kabila za wana wa Yakobo.Kisha akafanya mifereji ya maji kuyazunguka madhabahu kubainisha kuwa kile ambacho kingetokea kingekuwa muujiza na wala sio hila au ujanja kwa upande wake.Wakati Mungu alipotuma moto kutoka juu ukateketeza sadaka ya Eliya na kuni na kulamba maji yaliokuwa kwenye mfereji,wana wa Israeli hatimaye walifahamikiwa na uweza wa Mungu na kurudiwa na fahamu zao.-“
Na watu wote walipoona,wakaanguka kifudifudi;wakasema,Bwana ndiye Mungu,Bwana ndiye Mungu! ( 1 Wafalme 18:39)
Tunazo nguvu za ufufuo za Yesu Kristo kujenga moto ndani yetu,kutuosha na kututakasa.Tunapoifikia njia panda katika mwenendo wetu wa kiroho,tunap swa kumgeukia Mungu atupe mwelekeo sahihi.
Ombi:Baba ahsante ujasiri wa Eliya kuwakabili manabii wa Baali.Naomba unisaidie kufanya uamuzi ulio sawa ninapofikia njia panda.Nimeomba katika jina la Yesu.Amina.