Blessings Out of Blastings – SWA
“Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki;BWANA utamzungushia radhi kama” (Zaburi 5:12)
Kuna mzunguko ambao unaonekana katika maisha ya watu wa Mungu.Jinsi kijito cha Kerithi kilipokauka na kuhitimisha kipindi cha utulivu,msimu wa chakula tele huko Sarepta kwa Eliya ulitamatika.Majonzi yalishuhudiwa pale mwana wa yule mjane alipofariki na kuamsha chuki yake dhidi ya Mungu na Eliya.
( 1 Wafalme17:17-24)
Mzunguko wa Baraka ukifwatiwa na dhiki si jambo lisilo la kawaida miongoni mwa watu wa Mungu.Mara nyingi ufanisi hufwatiwa na majaribio makuu.Niliyashuhudia haya mwaka wa 1987 tulipoanzisha kanisa letu.Mungu alitubariki katika kila fani ambayo kanisa linaweza kubarikiwa kwayo.Watu 28 walihudhuria mkutano wetu wa kwanza kwenye chumba cha hoteli;idadi hiyo iliongezeka hadi watu 60 juma lililofwatia,huku waumini wenye bidii wakiendelea kumiminika pale.Nilikuwa nikikutana na watu asubuhi,mchana na usiku,huku nikijaribu kukabiliana na ongezeko kubwa la waumini.
Lakini ilipofika mwaka wa 1989 niliugua nimonia mara dufu,hivi kwamba nililoweza tu ni kujilaza kitandani.Mungu alikuwa akinificha jinsi alivyomfanya Eliya,huku akiniweka katika hali ya utulivu niweze kumsikiliza.Alinifundisha kuwa ningeliwahudumia tu wenzangu,ikiwa ningelimhudumia Mungu kwanza.Alinifundisha kuwa singeliweza kutenda lolote kwa nguvu zangu,lakini ningetenda yote kupitia Yeye.
Mungu ataleta Baraka bada ya kero kila wakati, iwapo tutaisikiliza sauti yake.
Ombi:Mungu ahsante kwa kumbusho la leo kwamba uko na baraka kwangu hata nyakati ngumu.Nisaidie nizingatie baraka leo.Ninaomba katika jina la Yesu.Amina.
Facing A Crossroads – SWA
“Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA,chagueni hivi leo mtakayemtumikia;kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngámbo ya Mto au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao;lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.” (Yoshua 24:15)
Katika kitabu cha 1 Wafalme 18 tunaona jinsi taifa la Israeli lilipokuwa limefikia njia panda.Halikumheshimu tena Mungu.Kwao,huyo Mungu alikuwa umbali wa maili mamilioni kadhaa.Japo waliendelea kusema ni wafwasi wa Yehova,lakini ukweli ni kwamba hakuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.Hata hivyo Mungu alijua kwamba alihitaji kuwakumbusha tu kuhusu uweza wake,ambao ungeliwaamsha kutoka kwenye usingizi wao wa kiroho.Kwa hivyo Mungu alimtumia Eliya kuleta mabadiliko katika maisha yao.Huku akikabiliwa na vipingamizi-mtu mmoja dhidi ya mamia ya viongozi wapagani-Eliya alidhihirisha bayana nguvu za Mungu.
Katika kitabu chicho hicho wa 1 Wafalme 18:22-39,watu walishuhudia ushindani wa ajabu.Kuliandaliwa mioto mara mbili tofauti ya kuni ,ambapo mafahali wawili waliokatakatwa waliwekwa juu yake kama sadaka ya kuteketezwa.Ni Mungu yupi aliyekuwa na uwezo wa kuasha moto kwenye mojawapo wa madhabahu hayo-Baali au Mungu wa Eliya?
Eliya kwa ujasiri mkuu uliotokana na imani katika Mungu mkuu,aliwatazama manabii 850 wapagani wakiomba miungu yao iwashe moto kwenye rundo lao kwenye madhabahu,lakini hapakuwaka moto.Eliya aliwakebehi na kuwaambia wawaite miungu wao kwa sauti ya juu labda wamelala!Kwa saa kadhaa manabii hao walipaaza sauti na hata kujikatakata kwa visu na vyembe na damu kuwachuruzika,lakini hapakutokea ishara ya moto.
Basi Eliya akatokea na kusogelea madhabahu yake ambako kulikuwa na dhabihu ya ng’ombe waliokatakatwa.Aliyafanyia matengenezo madhabahu hayo yaliokuwa yametelekezwa na wana wa Israeli.Aliyatwaa mawe kumi na mawili yalioakilisha kabila za wana wa Yakobo.Kisha akafanya mifereji ya maji kuyazunguka madhabahu kubainisha kuwa kile ambacho kingetokea kingekuwa muujiza na wala sio hila au ujanja kwa upande wake.Wakati Mungu alipotuma moto kutoka juu ukateketeza sadaka ya Eliya na kuni na kulamba maji yaliokuwa kwenye mfereji,wana wa Israeli hatimaye walifahamikiwa na uweza wa Mungu na kurudiwa na fahamu zao.-“
Na watu wote walipoona,wakaanguka kifudifudi;wakasema,Bwana ndiye Mungu,Bwana ndiye Mungu! ( 1 Wafalme 18:39)
Tunazo nguvu za ufufuo za Yesu Kristo kujenga moto ndani yetu,kutuosha na kututakasa.Tunapoifikia njia panda katika mwenendo wetu wa kiroho,tunap swa kumgeukia Mungu atupe mwelekeo sahihi.
Ombi:Baba ahsante ujasiri wa Eliya kuwakabili manabii wa Baali.Naomba unisaidie kufanya uamuzi ulio sawa ninapofikia njia panda.Nimeomba katika jina la Yesu.Amina.
God’s Strategies – SWA
“BWANA awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.” ( 2 Wathesalonike 3:5)
Eliya alileta mageuzi makubwa katika taifa la Isrel licha ya kwamba alikuwa mtu mmoja tu na raslimali chache.Yule mjane alifanya kitendo cha kipekee kwa kuwa alioka mkate na unga uliokuwa umesalia kwa ajili ya mtumishi wa Mungu na wala sio kwa ajili yake binafsi.Mungu huwapa jukumu la huduma ya kipekee mioyoni mwao,wale wampendao na hubariki uaminifu wao wanapopania kutekeleza mapenzi yake.
Mara nyingi mbinu za Mungu hazileti maana kwetu kwasababu,kinyume chake,upeo wetu wa maono ni mdogo sana.Wakati Mungu alipompeleka Eliya katika eneo la adui,Mungu alijua hapo ndipo mahala pa mwisho ambako askari wangelifika kumtafuta nabii huyo.Aidha Mungu alijua kuwa kwenda Sarepta kungelimwokoa Eliya kutokana na njaa,japo ilikuwa wazi kuwa kulikuwepo na janga la njaa nchini.Isitoshe na lililo muhimu kabisa ni kwamba Mungu alimdhihirishia Eliya kuwa aliwajali hata waabudu miungu akiwemo yule mjane na jamaa yake.
Mara nyingi pia Mungu huwa na malengo mseto na hufanya kazi katika mawanda tofauti wakati mmoja.Ikiwa tutafwata uongozi yake, tutabarikiwa na pia kufanyika vyombo vya baraka kwa wengine.
Je? Umeshawahi kuhimizwa na Mungu kutenda jambo ambalo kwako halileti maana wakati huo,lakini hayo ndio mapenzi yake? Je? Anakuhimiza uondoke kutoka mahala pako pa starehe ulipopazoea na kwenda usikojua? Labda ni jambo linalohusu fedha au taaluma yako? Unahisi unahimizika kutalii mawanda mengine tofauti katika huduma yako au katika mahusiano yako na Mungu?
Ombi:Mungu, mbinu zako za kutenda mapenzi yako wakati mwingine ni ngumu na hunikanganya,lakini nitatii mwito wako kwa sababu najua unaona kile ambacho mimi sioni.Ninaamini kuwa utanibariki na kunitumia kubariki wengine ninapokutii.Nimeomba katika jina la Yesu.Amina.
Principles of Powerful Prayer – SWA
“Lakini yeye alikuwa akijiepua,akaenda mahali pasiokuwa na watu akaomba” (Luka5:16)
Yakobo 5:17 inasema kuwa Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi,lakini alitekeleza wajibu muhimu ajabu kudhihirisha nguvu za Mungu katika historia ya Bibilia (Tazama Yakobo 5:16-18; 1 Wafalme 17:17-24,18:16-46)
Ni kipi kilimfanya Eliya kila wakati kupata matokeo yaliotarajiwa alipokuwa akikabiliana na wasioamini,maadui na viongozi wa kisiasa? Ni mtu wa aina gani Mungu anaweza kumtumia kama alivyomtumia Eliya? Kanuni sta muhimu zilimfanya Eliya kuwa na nguvu nyingi na ukaribu na Mungu.Leo tutachunguza tatu tu.
Kwanza,muitikio wa Eliya alipokutana na mjane huko Sarepta ni mfano bora wa kujikana na badala yake kumwacha Mungu ashike usukani.Wakati huyo mjane alipomshambulia kwa maneno makali,Eliya hakujitetea au kumpa mafundisho ya Biblia.Alichofanya nii kumchukua mtoto wake mikononi mwake na kujaribu kumsaidia.Alifahamu kwamba alikuwa akizungumza maneno hayo kutokana na uchungu wa kumpoteza mwanawe.Hali hiyo ilitokana na imani yake ya kipagani.Eliya hakutana kukinzana na imani yake bali aliacha Mungu ajitukuze katika hali hiyo.
Pili,Eliya alimuuliza Mungu maswali faraghani alipojifungia ili kuomba.Eliya alitembea na Mungu kwa ukaribu.Alijua kuwa Mungu alielewa utatanishi uliotokana na kifo cha mtoto wa huyo mjane,hata hivho alisubiri hadi wakati wake wa kuomba ndipo amuulize hayo maswali.Hakutaka kudhoofisha imani ya yule mjane na maswali aliokuwa nayo moyoni.
Tatu,Eliya alidumu katika maombi yenye hamasa.Aliomba mara tatu hadi roho ya mtoto ilipomrudia na akafufuka.Hakuwa na mpangilio wowote wa maombi bali aliendelea tu kuomba.
Ombi:Mungu,nakushukuru kwa mfano huo wa Eliya.Nisaidie ili niweze kuwa na kanuni za maombi ya kila siku katika maisha yangu.Nimeomba katika jina la Yesu.Amina.