Kanuni za maombi yenye nguvu
Principles of Powerful Prayer – SWA
“Lakini yeye alikuwa akijiepua,akaenda mahali pasiokuwa na watu akaomba” (Luka5:16)
Yakobo 5:17 inasema kuwa Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi,lakini alitekeleza wajibu muhimu ajabu kudhihirisha nguvu za Mungu katika historia ya Bibilia (Tazama Yakobo 5:16-18; 1 Wafalme 17:17-24,18:16-46)
Ni kipi kilimfanya Eliya kila wakati kupata matokeo yaliotarajiwa alipokuwa akikabiliana na wasioamini,maadui na viongozi wa kisiasa? Ni mtu wa aina gani Mungu anaweza kumtumia kama alivyomtumia Eliya? Kanuni sta muhimu zilimfanya Eliya kuwa na nguvu nyingi na ukaribu na Mungu.Leo tutachunguza tatu tu.
Kwanza,muitikio wa Eliya alipokutana na mjane huko Sarepta ni mfano bora wa kujikana na badala yake kumwacha Mungu ashike usukani.Wakati huyo mjane alipomshambulia kwa maneno makali,Eliya hakujitetea au kumpa mafundisho ya Biblia.Alichofanya nii kumchukua mtoto wake mikononi mwake na kujaribu kumsaidia.Alifahamu kwamba alikuwa akizungumza maneno hayo kutokana na uchungu wa kumpoteza mwanawe.Hali hiyo ilitokana na imani yake ya kipagani.Eliya hakutana kukinzana na imani yake bali aliacha Mungu ajitukuze katika hali hiyo.
Pili,Eliya alimuuliza Mungu maswali faraghani alipojifungia ili kuomba.Eliya alitembea na Mungu kwa ukaribu.Alijua kuwa Mungu alielewa utatanishi uliotokana na kifo cha mtoto wa huyo mjane,hata hivho alisubiri hadi wakati wake wa kuomba ndipo amuulize hayo maswali.Hakutaka kudhoofisha imani ya yule mjane na maswali aliokuwa nayo moyoni.
Tatu,Eliya alidumu katika maombi yenye hamasa.Aliomba mara tatu hadi roho ya mtoto ilipomrudia na akafufuka.Hakuwa na mpangilio wowote wa maombi bali aliendelea tu kuomba.
Ombi:Mungu,nakushukuru kwa mfano huo wa Eliya.Nisaidie ili niweze kuwa na kanuni za maombi ya kila siku katika maisha yangu.Nimeomba katika jina la Yesu.Amina.